HARGREVEAVES AMSHANGAA MOURINHO KUTOMPA NAFASI MKHITARYAN

Kiungo wa zamani wa kilabu ya Manchester United, Owen Hargreaves amemshangaa Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho kwa kutompa nafasi kiungo  Henrikh Mkhitaryan.

Mkhitaryan aliyesajiliwa msimu huu na miamba hao wa soka la Uingereza  akitokea Borussia Dotmund ya Ujerumani kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 26, ameweza kucheza mechi nne tu za ligi na mechi zote alizocheza amekuwa hachezi dakika 90.

Hargreaves anaamini kuwa kiungo huyo mwenye miaka 27 ana uwezo mkubwa wa kuweza kuleta mabadiliko kwenye kikosi cha Mourinho iwapo atapewa nasi.

Mkhitaryan aliumia  mwezi Septemba lakini sasa hivi amepona na anaonekana yuko tayari kwa ajili ya kucheza lakini Mourinho anampotezea jamabo linalomfanaya Hargreaves hashindwe kumuelewa kocha huyo Mreno.