MAN UTD HATIHATI KUMKOSA SMALLING WATAKAPOIVAA CHELSEA  UGENINI

Manchester United ipo kwenye hatihati ya kumkosa beki wake wake tegemeo Chris Smalling aliyeumia kwenye mechi ya jana dhidi ya Fenerbehce ambayo iliisha kwa United kushinda 4-1 wakiwa nyumbani.

Kocha wa kikosi hicho Jose Mourinho amewambia wanahabari kuwa alilazimika kumpumzisha Smalling dakika ya 46 na kumuingiza Marcus Rojo kutokana na beki huyo kuumia misuli.

Mourinho alisema kuwa hana uhakika kama beki huyo tegemeo katika kikosi chake atakuwa fiti siku ya Jumapili watakaposafiri kuifata Chelsea ya mjini London.

Hata hivyo kocha huyo ana matumaini ya kurejea kwa kiungo wake aliyesajiliwa msimu huu akitokea Borussia Dotmund, Henrikh Mkhitaryan. Mkhitaryan ambaye alikuwa majeruhi tangu alipoumia kwenye mechi dhidi ya Manchester City ameanza kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake na inawezekana akawepo kwenye kikosi kitakachosafiri kuifata Chelsea.

Mourinho na kikosi chake Jumapili watakuwa ugenini kwenye viunga vya Stanford Bridge kuikabili timu aliyoachana nayo msimu uliyopita Chelsea. Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 12;00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.