MAN UTD KUIVAA MAN CITY BILA ERIC BAILLY      

Manchester United watakuwa kwenye uwanja wao wa Old Traford kuwakaribisha mahasimu wao Manchester City katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini Uingereza, maarufu kama EFL.

Katika mchezo wa leo Manchester United itamkosa beki wake mahili Eric Bailly aliyesajiliwa msimu huu akitokea Valencia ya Uhispania.

Bailly alihumia goti kwenye mechi ambayo Man United ikiwa ugenini ilikubali kipigo cha 4-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Uingereza (EPL). Jeraha hilo litamuweka beki huyo raia wa Ivory Coast nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili.

Jose Mourinho akiwa na kikosi chake cha Man Utd, wataingia uwanjani wakiwa na kukmbukumbu ya kufungwa goli 2-1 na Man City ya Pep Guardiola kwenye mchezo wa Ligi Kuu (EPL).