MFARANSA KUWA MTENDAJI MKUU YANGA

Kilabu ya Yanga SC ya jijini Dar es salaam, imemuajili Mfaransa Jerome Dufourg kuwa mtendaji kuu wa kilabu hiyo yenye historia kubwa hapa nchini.

Dufourg ambaye amewahi kufanya kazi shirikisho la soka Rwanda (FERWAFA) anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote ili kumalizana na uongozi wa kilabu hiyo kwa ajili ya kuanza kazi.

Jukumu kubwa la kwanza kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 30, ni kuhakikisha mapato ya kilabu yanazidi matumizi. Matumizi ya Yanga mwaka jana ilikuwa shilingi Bilion 2.8 wakati iliingiza Bilioni 1.3 jambo linaloashiria kuwa ilikuwa ikijiendesha kwa hasara.

Tayari Yanga ipo kwenye mipango ya kubadili benchi zima la ufundi kwa kumuajili kocha Mzambia George Lwandamina atakayekuwa akisadiwa na mzawa Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa  yupo na timu ya Taifa, Taifa Stars.