POGBA APIGA MBILI MAN IKISHINDA 4-1 EUROPA

Mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba, jana aliifungia timu yake ya Manchester United mabao mawili kwenye mechi ya kundi ‘A’ katika michuano Europa League ambapo Man United iliibuka na ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Fenerbehce ya Uturuki.

Pogba alifunga goli lake la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 31 baada ya beki wa Feneberhce Simon Kjaer  kumwangusha kiungo mshambuliaji wa Man United  Juan Mata ndani ya kumi na nane. Pogba alifunga tena dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Jesse Lingard

Magoli mengine yalifungwa na Antony Martia dakika ya 34 ambaye pia alifunga kwa mkaju wa penati baada kufanyiwa faulo ndani ya kumi na nane na beki wa Fenerbehce Sener Ozbayrakli. Goli la nne lifungwa na Jesse Lingard dakika ya 48 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Wyne Rooney.

Goli la Fenerbehce lilifungwa dakika ya 83 na mshambuliaji Robin Van Persie ambaye pia amewahi kuichezea Man United. Van Persie alifunga goli hilo akimalizia kazi nzuri ya winga Mnigeria Emmanuel Emenike aliyewatoka mabeki wa United na kutoa pasi safi kwa mfungaji.

Mchezo mwingine kwenye kundi hilo ulizikutanisha Feyernood ya Uholanzi ambao walikuwa nyumbani kuwakaribisha  FC Zorya Luhansk ya Ukraine, mechi iliyoisha kwa Feyernood kuibuka na ushindi wa wa goli 1-0.

Kwa matokeo hayo Manchester United na Feyernood zote kwa pamoja zimefikisha pointi 6, lakini Feyernood anaongoza kundi ‘A’ kwa tofauti ya uwiano wa magoili ya kufunga na kufungwa Man United yupo nafasi ya pili. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Fenerbehce yenye point 4, na nafasi ya nne yupo Zorya yenye point 1.