YANGA KUANZA MAISHA MAPYA BILA PLUIJM

Na Victor Mahudi

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani.

Kikosi cha Yanga kitashuka dimbani bila kocha wake mkuu Hans Van Pluijm waliyedumu nae kwa kipindi cha miaka miwili.

Juzi Pluijm aliuandikia uongozi wa kilabu hiyo barua ya kujiuzulu baada ya kupata taarifa za Yanga kumuajiri kocha mpya bila kumjulisha.

Plujm alijiunga na yanga katikati ya msimu wa ligi wa 2014/2015 amabapo amekaa na timu hiyo kwa misimu miwili mfululizo na kuweza kuipa ubingwa wa ligi kuu mara mbili, kombe moja la Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho.

Mholanzi huyo ameondoka akiwa ameiongoza Yanga kupata ushindi mnono ugenini wa goli 6-2 dhidi ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera. Na kaiacha ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo chini ya Pluijm,  Juma Mwambusi ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu.

kumekuwa na habari za kilabu ya Yanga kuwa katika mchakato wa kubadili benchi zima la ufundi, ambapo taarifa za uhakika kutoka ndani ya kilabu hiyo zinabainisha kuwa Mzambia George Lwandamina ndiye atakuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu hiyo, ambapo atakuwa akisaidiwa na wazawa Boniface Charles Mkwasa kama kocha msaidizi, Peter Manyika kocha wa makipa na meneja Sekilojo Chambua