Nantes vs Marseille

Katika mchezo wa kushtua wa wiki hii, FC Nantes imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Marseille kwa kuwafunga mabao 3-0 katika uwanja wa La Beaujoire. Ushindi huu unawapa Nantes matumaini ya kukwepa kushuka daraja, wakati Marseille ikikosa fursa ya kusogea karibu na nafasi za juu.