Paris Saint-Germain imelazimishwa sare ya 2-2 na FC Lorient katika uwanja wa Parc des Princes. Kinda Ibrahim Mbaye alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 6, akionyesha kwanini Luis Enrique anamuamini. Licha ya PSG kutawala umiliki wa mpira kwa zaidi ya asilimia 80, safu ya ulinzi ya Lorient ilikuwa imara kuzuia mashambulizi ya Ousmane Dembélé na Bradley Barcola.