Paris Saint-Germain imekamilisha usajili wa kiungo kijana wa Kihispania, Dro Fernandez (18), kutoka Barcelona kwa mkataba wa hadi mwaka 2030. Usajili huu wenye thamani ya €8.2 milioni ni sehemu ya mkakati wa klabu kuwekeza kwa wachezaji chipukizi wenye vipaji vikubwa.